Nenda kwa yaliyomo

Ugonjwa unaoshambulia kingamwili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ugonjwa unaoshambulia kingamwili
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuWataalamu wa magonjwa ya baridi yabisi, magonjwa ya mfumo wa kingamwili (immunology), magonjwa ya tumbo (gastroenterology), magonjwa ya mfumo wa neva (neurology), ugonjwa wa ngozi (dermatology)
DaliliInategemea na hali ya ugonjwa. Kwa kawaida, homa ya kiwango cha chini, kuhisi uchovu[1]
Muda wa kawaida wa kuanza kwakeUtu uzima[1]
DawaDawa za kupunguza uvimbe zisizo za asteroidi, dawa za kukandamiza mfumo wa kingamwili, immunoglobulini inyowekwa mishipani[1][2]
Idadi ya utokeaji wakeWatu milioni 24 / asilimia 7% (Marekani)[1][3]

Ugonjwa unaoshambulia kingamwili (kwa Kiingereza: autoimmune disease) ni hali inayotokana na mwitikio usio wa kawaida wa kinga kwa sehemu ya mwili inayofanya kazi.[1] Kuna angalau aina 80 za magonjwa yanayoshambulia kingamwili.[1] Karibia sehemu yoyote ya mwili inaweza kuhusika.[3] Dalili za kawaida ni pamoja na homa ya kiwango cha chini na kuhisi uchovu.[1] Mara nyingi dalili hutokea na utoweka.[1]

Kisababishi kwa ujumla hakijulikani.[3] Baadhi ya magonjwa yanayoshambulia kingamwili kama vile lupasi hutokea katika familia na visa vingine vinaweza kuchochewa na maambukizo au sababu nyingine za kimazingira.[1] Baadhi ya magonjwa ya kawaida ambayo kwa ujumla huzingatiwa kama magonjwa yanayoshambulia kingamwili ni pamoja na ugonjwa wa siliaki (celiac), kisukari aina ya 1, ugonjwa wa Graves, ugonjwa wa kuvimba kwa mfumo wa chakula, ugonjwa wa kushambulia neva za mwili (multiple sclerosis), ugonjwa ya ngozi (psoriasis), ugonjwa wa baridi yabisi (rheumatoid arthritis), na ugonjwa wa mfumo wa kinga ya mwili (systemic lupus erythematosus).[1][4] Utambuzi wake unaweza kuwa mgumu kubaini.[1]

Matibabu yanategemea aina na ukali wa hali hiyo.[1] Dawa za kupunguza uvimbe zisizo za steroidi (NSAIDs) na dawa za kukandamiza kingamwili hutumiwa mara nyingi.[1] Immunoglobulini inayowekwa mishipani inaweza pia kutumika mara kwa mara.[2] Ingawa matibabu kwa kawaida huboresha dalili, hazitibu ugonjwa huo kwa kawaida.[1]

Takriban watu milioni 24 (asilimia 7) nchini Marekani wanaathiriwa na ugonjwa unaoshambulia kingamwili.[1][3] Wanawake huathiriwa zaidi kuliko wanaume.[1] Mara nyingi huanza katika utu uzima.[1] Magonjwa ya kwanza yanayoshambulia kingamwili yalielezewa mapema miaka ya 1900.[5]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 "Autoimmune diseases fact sheet". Office on Women's Health. U.S. Department of Health and Human Services. 16 Julai 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 5 Oktoba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Katz U, Shoenfeld Y, Zandman-Goddard G (2011). "Update on intravenous immunoglobulins (IVIg) mechanisms of action and off- label use in autoimmune diseases". Current Pharmaceutical Design. 17 (29): 3166–75. doi:10.2174/138161211798157540. PMID 21864262.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Borgelt, Laura Marie (2010). Women's Health Across the Lifespan: A Pharmacotherapeutic Approach (kwa Kiingereza). ASHP. uk. 579. ISBN 978-1-58528-194-7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-08.
  4. Hohlfeld R, Dornmair K, Meinl E, Wekerle H (Februari 2016). "The search for the target antigens of multiple sclerosis, part 1: autoreactive CD4+ T lymphocytes as pathogenic effectors and therapeutic targets". The Lancet. Neurology. 15 (2): 198–209. doi:10.1016/S1474-4422(15)00334-8. PMID 26724103.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Ananthanarayan R, Paniker CK (2005). Ananthanarayan and Paniker's Textbook of Microbiology (kwa Kiingereza). Orient Blackswan. uk. 169. ISBN 9788125028086. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-08.